Bayo ni moja ya msanii ambaye amekuwa kaifanya vizuri kutoka nchini Tanzania akiwa anawakilisha mziki wa dancehall akiwa pia anawakilisha mkoa wa Mwanza.
Amefanikiwa kufanya kazi nyingi tofauti tofauti lakini pia moja ya kazi yake ambayo imefanikiwa kuchukua nafasi kubwa n ahata kuingia katika chati tofauti tofauti za muziki ni Pamoja na wimbo wake wa nampenda ambao bado unaendelea kufanya vizuri.
Akifanya mahojiano kupitia kipindi cha hitzone ndani ya jembe fm Bayo aliulizwa mtazamo wake kuhusu ukumbwa wa muziki wa dancehall na singeli Tanzania na liweka wazi kuwa”
Kiuhalisia singeli ni muziki ambao umekuwa na mapokeo makubwa kulinganisha na dancehall singeli imepewa nafasi n ahata baadhi ya vituo vya redio kuutambulisha mziki hio kama kitambulisho chao n ahata kupata ukubwa katika majukwaa mbali mbali japo kuwa muziki wa dancehall Tanzania kuna makubwa yanakuja mashabiki wasubiri tu kuona mabadiliko”
Alisema Bayo ambaye pia ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Dodoma ukiwa unazungumzia maeneo mbali mbali .