Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalaama Barabarani yatakayofanyika Mkoani Mwanza Kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewaambia waandishi wa habari Jijini Mwanza maadhimisho hayo yatafanyika March 14, 2023. Ikiwa ni lengo la kuendelea kutoa elimu ya sheria, Kanuni na taratibu za usalama barabarani kwa makundi yote ya watumiaji wa barabara.
Maadhimisho hayo yataongozwa na kaulimbiu isemayo "Tanzania bila Ajali inawezekana - Timiza wajibu wako"
Mkuu wa Mkoa Malima amesema kauli mbiu hii inasisitiza kuwa kila mtumiaji wa barabara akitimiza wajibu wake kutapelekea kupungua kwa ajali za barabarani na hatimaye kuhimarika kwa usalama barabarani.
Aidha Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani nchini SACP. Ramadhan Ng'anzi amesema madhimisho hayo itakuwa ni fursa ya ukaguzi wa vyombo vya usafiri ikiwemo pikipiki, Bajaji na Magari na baadae kutoa vyeti maalumu vitakavyo ononesha vyombo hivyo vinafaa kwa ajili ya matumizi ya Barabarani.
Hata hivyo Wanachi ndani na nje ya mikoa ya Mwanza wameaswa kujitokeza kushiriki maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya Furahisha vilivyopo Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza.