Tume ya Uchaguzi Yatangaza Majimbo Mapya 8 na Kubadili Majina ya Majimbo 12

Tume Huru ya Uchaguzi imetangaza mabadiliko makubwa ya kiutawala katika mipaka ya majimbo ya uchaguzi nchini, ikiwemo mabadiliko ya majina ya majimbo 12 na kuanzishwa kwa majimbo mapya 8.

Kwa mujibu wa taarifa ya tume, majimbo hayo mapya yameanzishwa kutokana na kugawanywa kwa baadhi ya majimbo yaliyokuwa na ukubwa mkubwa au ongezeko la watu, hatua inayolenga kuboresha uwakilishi wa wananchi.

Majimbo mapya yaliyoanzishwa ni kama ifuatavyo:

Majimbo Mapya ya Uchaguzi: Kivule lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Ukonga, Mkoa wa Dar es Salaam na Chamazi – lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbagala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Mengine ni Mtumba lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Dodoma Mjini, Mkoa wa Dodoma, Uyole lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya na Bariadi Mjini lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Pia lipo Katoro lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Busanda, Mkoa wa Geita, Chato Kusini lilioanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Chato, Mkoa wa Geita na Utwangi lililoanzishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Solwa, Mkoa wa Shinyanga.

Tume imesema mabadiliko haya ni sehemu ya maboresho ya mipaka ya kiutawala ili kuhakikisha uwiano wa idadi ya watu kwenye majimbo ya uchaguzi na ufanisi wa uwakilishi wa wananchi bungeni. Na Elvan Stambuli GPL

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii