Watumishi wahimizwa kuzingatia maadili serikalini

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Jacob Rombo amewasihi watumishi wa Wizara ya Ujenzi kuzingatia maadili ya kutunza siri za Utumishi wa Umma kwa kuzingatia kanuni, taratibu na Miongozo iliyowekwa na Serikali ili kufanikisha huduma bora za ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja kwa jamii.

Rombo ameeleza hayo leo Julai 01, 2025 Mkoani Arusha wakati akifungua mafunzo ya Huduma kwa Mteja katika mazingira ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma yanayotolewa na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yanayofanyika Mkoani humo.

“Sisi kwenye maeneo yetu ya kazi ambayo tumeamianiwa, tuhakikishe tunafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kutokuwa chanzo cha utoaji wa siri za Serikali.

Amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo ya kiutendaji ya utumishi wa umma ya mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea kuwafundisha na kuwakumbusha watumishi wa umma wajibu wao wanaopaswa kufanya.

Aidha, Rombo amepongeza Uongozi wa Wizara ya Ujenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mbalimbali iliyokamilika na ile inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali kwa kuwa miradi hiyo inaleta tija kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo hayo, Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi Bw.Onesmo Mkandawile ameeleza kuwa mafunzo hayo ni utekelezaji wa mpango wa mafunzo wa Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Mkandawile ameeleza kuwa mafunzo hayo yalianza mwezi Januari, 2025 na yamefanyika kwa awamu kwa lengo la kuhakikisha watumishi wote wa Wizara wanafikiwa na wanapatiwa mafunzo hayo.

Naye Mhadhiri wa Mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Bw. Emmanuel Masewa ametaja mada mbalimbali zitazofundishwa zikiwemo maadili, Rushwa na Uwajibikaji katika Utumishi wa Umma, Mawasiliano ya Kiofisi na Utunzaji wa Siri za Ofisi na Huduma kwa Mteja.

Mada nyingine zitakazofundishwa ni Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 8 ya 2002 RE 2019, Kanuni za Utumishi wa Umma 2022, Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma 2009, Magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza, Akili ya Kihisia pamoja Msongo wa Mawazo na A

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii