DTO atoa mkakati wa kuanza kupima madereva kila wikendi

Leo julai mosi kwenye Kipindi cha MchakaMchaka amesikika Mkuu  Usalama Barabarani Wilaya ya Ilemela DTO Kilimbida Thomas Kilimbida na kueleza mkakati madhubuti wa kuanza kupima madereva katika siku za mwisho wa wiki,  ndani ya maeneo ya kumbi za starehe ikiwa   lengo ni kuendelea kudhibiti ajali za baranbarani.

Ameeleza hayo  kufuatia ajali iliyotokea Moshi - Tanga, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kwa magari mawili kugongana na kuungua moto na ajali iliyotokea eneo la Kona ya Ulinji,nje kidogo ya Mji wa Sumbawanga Mkoani Rukwa huku baadhi ya abiria wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Amesema baadhi ya maeneo katika Wilaya ya Ilemela bado inachangamoto ya uzembe ndogondogo kwa  baadhi ya madereva ikiwa pamoja na kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa hali ambayo imepelekea kuanzishwa kwa mkakati  huo.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii