“Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, imeipa Yanga sehemu ya ardhi yake hapa Jangwani kwa ajili ya kujenga uwanja wa Yanga, na miezi michache ijayo mtaona zoezi la ujenzi wa uwanja wetu likianza." Amesema Eng. Hersi Said.