Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa Mhe. Vladimir Putin

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Urusi, Mhe. Vladimir Putin, kwa kuadhimisha Siku ya Ushindi (Victory Day) tarehe 9 Mei 2025.

Katika salamu hizo, Rais Samia amepongeza ushupavu, mshikamano, na kujitolea kwa wananchi wa Urusi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, akisema kuwa ushindi wao ulikuwa wa kihistoria na wa gharama kubwa. Aidha, amepongeza uhusiano wa kirafiki na wa heshima kati ya Tanzania na Urusi, akisisitiza kuwa kumbukumbu ya siku hiyo inaendelea kuhamasisha dunia kudumisha amani, haki, na ushirikiano.

Rais Samia amemtakia Rais Putin na wananchi wa Urusi mafanikio, amani na ustawi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii