Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Ramadhan Missiru kujihusisha na masuala ya mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 6 na kulipa faini ya Tsh milioni tano baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili.
Taarifa ya leo Mei 13, 2025 iliyotolewa na TFF imeeleza makosa hayo ambayo ni kushindwa kutii uamuzi wa Kamati ya Maadili ya TFF kinyume na Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2021 na kosa la kuchochea umma kinyume na ya Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2021 ambapo adhabu hiyo dhabu hiyo imeanza tarehe 8 Mei 2025.