Polisi yawataka Waendesha Baiskeli kutii sheria usalama barabarani

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limewataka waendesha baiskeli mkoani humo kutii sheria za usalama barabarani bila kushurutishwa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Sammy Magige wakati akifungua mazoezi ya waendesha baiskeli yaliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara ikiwemo baiskeli ya namna ya utumiaji sahihi wa vyombo hivyo wakiwa barabarani.

Akiongeakwa niaba ya waendesha Baiskeli wenzake, Ramadhan Athumani amesema wameungana ili kupaza sauti kwa jamii kupata uelewa wa pamoja kuhusu haki ya matumizi ya barabara bila kubaguana akitolea mfano watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki na hata magari.

Awali, Sajenti Atilio Choga toka Dawati la Elimu kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha amesema kila mmoja akitimiza wajibu wake barabarani bila kushurutishwa kwa kufuata sheria itapunguza na kuondosha ajali.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii