Spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy anasema hana mpango wowote wa kuizuru Ukraine baada ya Rais Volodymyr Zelenskiy kumpa mwaliko.
Haya ni kwa mujibu wa shirika la habari la Marekani CNN. Katika mahojiano na shirika hilo la habari, McCarthy amesema hahitaji kwenda Ukraine kujionea mambo yalivyo badala yake anaweza kupata taarifa kwa njia nyengine.
Msimamo wa spika huyo ni kwamba anaiunga mkono Ukraine katika vita dhidi ya Urusi ila Warepublican waliochukua udhibiti wa bunge hilo mnamo mwezi Januari, hawatatoa uhuru wa Marekani kuisaidia Ukraine.
Marekani imeipa Ukraine msaada wa takriban dola bilioni 32 tangu Urusi ianze uvamizi wake mnamo Februari 24 mwaka jana, ila baadhi ya Warepublican wenye siasa kali za mrengo wa kulia wamekataa kuitumia Ukraine msaada zaidi.