Baraza la Kitaifa la Kupambana na Magonjwa Sugu (NSDCC), limefichua kuwa asilimia 18.2 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimbi yanatokana na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao.
Kulingana na ripoti ya NSDCC 2022, wanaume 61,650 ambao walifanya mapenzi na wanaume wenzao walichangia maambukizi mapya ya VVU katika muongo mmoja uliopita.
Ripoti hiyo pia ilifichua kuwa wale wanaojitambulisha kama waliobadilisha jinsia walirekodi maambukizi mapya ya VVU 4,370 huku makahaba wenye maambukizi mapya wakiwa 197,096. Vile vile, maambukizi mapya 26,673 yalirekodiwa kati ya watu wanaojidunga dawa za kulevya.