CCM yasogeza mbele uchaguzi wa Sekretarieti

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesogeza mbele uchaguzi wa viongozi wa Sektetarieti ya Halmshauri Kuu ya chama hicho hadi itakapotangazwa tena.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Dodoma baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka amesema kwa sasa viongozi wa Sekretarieti waliopo wataendelea na majukumu yao.

Kila baada ya kipindi cha miaka mitano, Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo wale wa Sekretarieti Kuu.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii