Watu wengi huota kuwa wafanyabiashara wakubwa, lakini si wote wanaochukua hatua za kweli za kuanza na kudumu. Hii ni hadithi ya kijana wa Kitanzania, anayejulikana kwa jina la Aisam Magari, ambaye ameandika jina lake kwenye orodha ya wauzaji magari wanaoaminika zaidi nchini Tanzania.
Aisam alianza kama freelancer mdogo, akiuza laini za Tigo zamani sasa ni YAS mitaani. Hakuna aliyempa jukwaa aliamua kulijenga mwenyewe. Alijifunza kushughulika na watu, kuelewa mahitaji yao, na kuamini katika juhudi binafsi.
Kutokana na nidhamu, uthubutu, na ufuatiliaji, alianza kujipatia mtaji wa kuanzisha biashara ya magari. Leo hii, Aisam Magari si jina tu, bali ni nembo ya kuaminika katika soko la magari nchini.
Leo hii, biashara ya Aisam imepanuka hadi katika mikoa mbalimbali, ikiwa na ofisi rasmi zenye wafanyakazi zaidi ya 36. Kila mmoja ana nafasi yake, ana majukumu yake, na analipwa kwa stahiki zake hii ni ndoto ambayo sasa imegeuka kuwa chanzo cha riziki kwa familia nyingi.
Katika dunia ya sasa, teknolojia ni mkombozi. Aisam analitambua hili. Ndiyo maana katika kila ofisi yake, kuna router kutoka Yas inayohakikisha biashara inaendelea kwa kasi bila kikomo.
Kupitia kamera za usalama zilizounganishwa na mtandao, Aisam anaweza kufuatilia shughuli zote hata akiwa safarini. Hii ni biashara ya kisasa, inayokwenda sambamba na wakati.
Kwa sasa, Aisam ndiye muuzaji wa magari mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii Tanzania. Amekuwa mfano halisi wa jinsi mtu anavyoweza kuitumia TikTok, Instagram, na Facebook sio kwa burudani tu, bali kama majukwaa ya kuuza na kujitangaza.
Aisam anawakumbusha vijana wote kuwa mafanikio hayaji mara moja, bali yanaanza pale ulipo, kwa kile kidogo ulicho nacho. Kwa mfano wake, anathibitisha kuwa si lazima uwe na mtaji mkubwa kuanza biashara, bali lazima uwe na nia, bidii, na uthubutu.