Serikali yaendelea kuboresha mazingira rafiki kwa wafanya biashara

Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa urahisi, ufanisi na gharama nafuu.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 10, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji, Baraka Aligaesha akimwakilisha Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Dk Tausi Kida amesema Serikali imechukua hatua madhubuti kuondoa changamoto zinazokwamisha uwekezaji na biashara nchini.

Amebainisha kuwa Serikali imepunguza au kuondoa baadhi ya tozo zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara sambamba na kufanya marekebisho ya sheria na kanuni mbalimbali kwa kuzingatia maoni ya wadau pia imeanzisha mifumo ya kidijitali kurahisisha utoaji wa leseni na vibali.

Aidha vitengo maalum vimeanzishwa katika halmashauri kwa lengo la kuhamasisha biashara na kutatua changamoto za wafanyabiashara kwa wakati. Aligaesha ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali kuimarisha uchumi wa Taifa.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii