YAS ANZIA ULIPO :TUPOKIGWE AMBWENE KUTOKA MASTERS YA UTANGAZAJI HADI KUUZA MAKANDE POINT.

Katika dunia ya leo ambapo mafanikio hupimwa kwa vyeo, mshahara mkubwa na umaarufu, kuna hadithi chache sana zinazobeba uzito wa uhalisia kama ya Tupokigwe Hii ni hadithi  ya kuacha kazi ya kifahari, kurudi chini kabisa, na kugundua kuwa wakati mwingine, safari ya kweli ya ndoto huanza pale ambapo wengi hawathubutu kuangalia.

Kama ilivyo kampeni ya YAS Anzia Ulipo Usiogope Mwanzo Mdogo

Nina masters ya Mass Communication. Nimefanya kazi kwenye televisheni kama mtangazaji kwa zaidi ya miaka kumi, na pia nikafanya kazi katika shirika la kimataifa la Voluntary Service Overseas (VSO), Geita. Kila mtu alifikiri “amefika”, lakini ndani yangu kulikuwa na pengo lisilojazwa na mshahara au umaarufu. Ndoto yangu ilikuwa uhuru wa kifedha na kufanya kitu chenye maana kwa nafsi yangu.

Safari Iliyokuwa Sawa na Kutangatanga Haikuwa rahisi. Nilijikuta nikiruka kutoka kazi moja hadi nyingine, biashara moja hadi nyingine nikitafuta jibu la swali moja kubwa: “Nitawezaje kutimiza ndoto zangu bila pesa nyingi?”

Kama ilivyo kwa vijana wengi, nilikuwa ninasema:

“Nikipewa milioni tano, au milioni kumi, nitaanza biashara yangu, nitasimama.”

Lakini nilipojiuliza kwa kina:

“Kwenye hizo milioni tano, nitaweka flame, nitanunua bidhaa, nitaweka mapambo lakini kweli hizo ndizo zinanikwamisha?”

La hasha. Kinachotuzuia siyo ukosefu wa pesa ni woga. Ni mfumo wa malezi na jamii unaotufundisha kusubiri msaada badala ya kuamini kuwa tunaweza kuanza na kidogo tulicho nacho.

Kuamua Kuwa Huru Hata Kama Ni Kwa kuuza Makande Na ndio, nilichukua hatua ya ujasiri. Nilijitoa kwenye kazi za ofisini, na leo hii nauza makande.


Lakini haya si makande ya kawaida. Haya ni matokeo ya maono, uthubutu, na ushuhuda kuwa unaweza kuanza popote ulipo. Naweza kusema kwa fahari, kwa uhuru, na kwa amani moyoni kwamba niko kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto zangu.

Nilipopata nafasi ya kujiunga na mtandao wa Yas, ndipo nikagundua nguvu ya TikTok na Instagram kama silaha za biashara ya kisasa niliweza kugeuza content ndogo ndogo kuwa mazungumzo makubwa.

Leo video zangu zinaleta wateja. Makande yangu yanaenda mbali zaidi ya mtaa yanafika kwenye simu yako.

Kupitia Yas, nimejifunza jinsi ya kutumia hadithi yangu kama bidhaa. Na sasa siuzi tu makande, nauza lifestyle.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii