Kwenye familia ya Nyanda , maisha yalizunguka kwenye jambo moja kuu ufugaji na kilimo Hilo ndilo jambo lililopewa uzito kuliko chochote kingine. Biashara, teknolojia, au ndoto nyingine yoyote yalionekana kama mambo ya kupoteza muda. “Kitu ambacho wanaamini kwenye familiyetu ni ufugaji,” anasema Nyanda. “Hawaamini biashara, hawaamini vitu vingine.”
Hali hiyo ilimfanya kukua kwenye mfumo uliofungika. Maisha yalikuwa ya kazi na majukumu ya kila siku, na kwa kuwa alikuwa kijana wa kijijini, nafasi za kuona dunia nje ya kijiji zilikuwa finyu. “Mimi nilikuwa nikipata nafasi siku za weekend nakwenda mjini ,” anasema – akimaanisha kwamba muda wake mwingi uliishia katika majukumu ya nyumbani, huku weekend pekee akiwa na nafasi ndogo ya kuwa kijana.
Lakini kila safari kubwa huanza na hamu. Alipoenda mjini kwa mara ya kwanza, alikutana na marafiki waliomfungulia macho. “Unakuta wanaangalia, wanaperuzi huko TikTok. Na mimi nawaona wale maarufu Wanatrendi kipindi hicho. Nilitamani kile kitu.”
Lakini Nyanda hakuwa tayari kurudi nyuma. Alijua alichokitaka. “Siku jali sana. Nikasema, ‘Jamani kwa sababu mmeniambia, haina shida .’” Akaamua kupiga moyo konde na kuendelea.
Kupitia simu hiyo hiyo aliyoipiganiwa, akaanza kurekodi klipu. Aliweka kwenye TikTok bila kujua hata nani anaangalia. “Kipindi hicho mimi viewers sijui. Sijui watu wamefikia wangapi. Ilikuwa tu, nikirekodi kitu, lazima Tanzania nzima waone!”
Safari yake haikuwa ya kifahari, lakini ilikuwa na lengo. Aliamini kwamba sauti yake inaweza kusikika, hata kama anatoka kijijini. Na leo, Nyanda Kabudi, anayejulikana pia kupitia kampeni ya YAS amekuwa mfano hai wa jinsi mtu anaweza kuanzia alipo bila mitaji mikubwa, bila support ya familia na kutumia teknolojia kama daraja la kufikia ndoto zake.Leo hii, sauti yake, hadithi yake, na maudhui yake yanawagusa maelfu, kama si mamilioni, kwenye mitandao ya kijamii. Kile kilichoonekana kama ‘simu ya kupoteza muda’ kiligeuka kuwa zana ya kubadilisha maisha.