Mhamasishaji wa mtandao wa Tiktok nchini Kenya anayeshtumiwa kwa kuchochea vurugu dhidi ya maafisa wa polisi amekamatwa jijini Nairobi.
Mtuhumiwa huyo aliyetambuliwa kama Godfrey Mwasiaga Kakan Maiyo alichukuliwa na maafisa wa DCI baada ya video iliyowekwa kwenye akaunti yake ya Tiktok kusambaa mitandaoni iliyodaiwa kutoa wito wa mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama.
Mamlaka zilisema kukamatwa huko ni sehemu ya msako mkali dhidi ya watu wanaotuhumiwa kueneza chuki na kuchochea machafuko katika maandamano ya hivi majuzi yaliyopinga serikali.