Ruto atoa maagizo polisi kuwapiga risasi za miguu waandamanaji

Rais wa Kenya William Ruto ameagiza Polisi kuwapiga risasi za miguu waandamanaji wanaoharibu mali za watu ili kuwazuia kufanya uharibifu huo bila kuwaua.

Agizo hilo limekuja baada ya baadhi ya waandamanaji kuvamia maduka na ofisi na kuiba pamoja na kuharibu bidhaa kwenye maandamano yaliyofanyika Julai 7, 2025 

Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) na Mashirika ya Haki za Binadamu, yaliishutumu Polisi kwa matumizi makubwa ya nguvu katika Maandamano yanayojiri kuipinga serikali ya Kenya ambapo katika Maandamano ya 77 watu 31 waliripotiwa  kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa 

Kenya katika kipindi cha karibuni imekumbwa na wimbi la maandamano yanayodai kuondoka kwa Rais Ruto madarakani, yakiongozwa na kauli maarufu ya “Ruto must go” ambapo waandamanaji wanalalamikia hali ngumu ya maisha, ongezeko la kodi, pamoja na ukatili unaofanywa na Polisi kwa wananchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii