Kesi namba 8323/2025 ya mgawanyo wa rasilimali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 14, Julai 2025 saa nne asubuhi
Katika Kesi hiyo inayoendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam, mawakili wa upande wa waleta maombi wameiomba mahakama kupata muda wa kwenda kuisoma na kutafakari barua iliyopelekwa mahakamani hapo na upande wa wajibu maombi (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu).
Kuahirishwa kwa shauri hilo kunaathiri maombi yaliyowasilishwa mahakamani na upande wa CHADEMA ya kuiomba mahakama kufuta uamuzi alioutoa Jaji Mwanga Juni 10, juu ya kusimamishwa kwa shughuli za CHADEMA