CHAUMMA kuja na awamu ya pili ziara ya Chopa siku 13

Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA), kimetangaza awamu ya pili ya ziara yake baada ya ile iliyofanyika Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, John Mrema, ziara hiyo itaanzia Zanzibar ikiongozwa na Mwenyekiti wa wake taifa, Hashimu Rungwe pamoja na viongozi wengine wakuu akiwamo Katibu Mkuu wake, Salum Mwalimu.

Mrema amesema ziara hiyo itatumia usafiri wa Helkopita(CHOPA) pamoja na usafiri wa magari na viongozi watakaokuwapo katika ziara hiyo watagawanyika katika makundi mawili.

Ametaja mikoa mingine itakayopitiwa na ziara hiyo kuwa ni Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Dodoma, Singida, Mbeya na Rukwa.

“Na kama kawaida yetu ziara yetu itakuwa ya Chopa, hivyo wale waliokuwa wanadhani kwamba tumeishiwa pumzi, tunakwenda na ratiba yetu, hatuendi na ratiba za watu. Na kwa kwa awamu hii tutajigawa timu mbili, moja ardhini na nyingine angani wa sababu maeneo ya kufika ni mengi na muda ni mfupi."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii