Msanii wa Kenya Nameless na mke wake Wahu Kagwi wamebarikiwa kupata mtoto wa tatu wa kike wiki tatu zilizopita na mshabiki wake wakitaka wapate mtoto wa kiume.
Moja ya shabiki aliandika kwenye mitandao ya kijamii "Tafuta kijana boss...your legacy...we Africans." nae Nameless aliamua kujibu sisi ni Waafrika, tunapaswa kujua kuna mila zilizopitwa na wakati na sisi ni wanadamu hatupaswi kuishi kwenye kasumba ya tamaduni ambazo zinadunisha jinsia fulani iwe mtoto wa kike au wa kiume katika jamii kwa kuwa wote ni sawa.