MBUNGE AFICHA MAGONGO YA MWENZAKE NCHINI KENYA

Katika hali ya kushanganza Mbunge mmoja wa jimbo la Embakasi Mashariki nchini Kenya aliyefahamika kwa jina Babu Owino amezua taharuki bungeni baada ya kuficha magongo ya kutembelea ya mbunge mwenzake David Sankok na kusababisha shughuli za bunge kusimama kwa muda.

Wabunge hao walikuwa wamekusanyika katika majengo ya Bunge kujadili mapendekezo ya mabadiliko yenye utata katika Sheria ya Vyama vya Kisiasa,ambapo katikati ya kikao hicho Sankok alishtuka kwamba magongo yake hayapo.

Naibu Spika Moses Cheboi alilazimika kusimamisha kwa muda kikao hicho na kuanza msako wa kuwatafuta magongo yaliyotoweka ambapo muda mfupi baadae Owino alijitokeza wazi na kukiri kuwa ni kweli amehusika kuficha magongo hayo ili kuwafurahisha wabunge wengine

Baada ya kubainika kuwa ndiye mhalifu,Mbunge huyo wa Embakasi Mashariki baadaye aliagizwa kuomba radhi Bunge kwa hatua yake aliyoifanya

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii