Msanii wa Bongo Fleva Queen Darleen aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ya Diamond Platnumz ambaye ameibuka kusema kwamba acha watu wamuone mjinga baada ya kuachana na ndoa.
Darleen ambaye alifunga ndoa na mfanyabiashara Isihaka Mtoro kabla ya mambo kwenda mrama anasema kuwa, baada ya kuchukua hamsini zake, kwa anaishi maisha yenye furaha kuliko wakati alipokuwa ameolewa.
Darleen amesema hayo wakati akitoa maoni yake kuhusu habari ya kusikitisha ya mwanamke wa Nigeria aliyefariki dunia wakati akikimbizana kwa gari na mume wake aliyekuwa na mchepuko ndani ya gari linguine.