Ajali ya Iringa Waliofariki wafika kumi.

Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali iliyotokea jana katika eneo la Lungumba Kata ya Mahenge karibu na mlima Kitonga mkoani Iringa imeongezeka na kufikia kumi.

Majeruhi mmoja kati ya watatu waliotokana na ajali hiyo, amefariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ilula.

Ajali hiyo ilihusisha gari ya magazeti aina ya hiace, iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kuacha njia na kugonga mti.

Majerihi wawili waliobaki ambao ni dereva wa pili (alikaa kushoto), Hussein Issa Ally na Monica Philly, raia wa Malawi wamehamishiwa katika Hospitali ya Rifaa ya Mkoa wa Iringa wakiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kifo cha majeruhi wa kumi na kwamba miili yote imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii