Watu wawili wamefariki akiwemo kijana aliyeuawa kwa kukatwa na panga baada ya kufumaniwa na mke wa mtu kilimanjaro. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema jana kuwa mwanamke aliyefumaniwa na kijana huyo alijiua kwa sumu.
“ Anna Shirima (26) na Juvenal Peter (23) walifumaniwa Desemba 4 mwaka huu saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Kibaoni, Kata ya Nanjara wilayani Rombo katika mkoa huo”
“Baada ya fumanizi mwanaume alicharangwa mapanga na mume wa dada huyo hadi kifo lakini mwanamke kutokana na fedheha ya tukio hilo naye alikunywa sumu na alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Huruma Rombo,” alisema.Kamanda Maigwa