Wakazi atangaza ujio wa album yake ya tatu #Beberu

Kupitia mitandao yake ya kijamii Wakazi ametangaza ujio wa album hiyo baada ya album ya Live at Sauti za Busara ambayo ndio ilikuwa album yake ya mwisho aliyoiachia mwaka 2021.

Endapo Wakazi ataachi album hiyo basi itamfanya rapa huyo kuwa na jumla ya album tatu ingawa aliachia EP ya Abacus ya mwaka 2014  ambayo ilikuwa na ngoma nne yaani Weekend, Touch, Sumu ya panya na Wanawake wa Dar.

Album ya kwanza ya Wakazi ilikuwa Kisimani ya mwaka 2018 ambayo ilikuwa na ngoma 18 na kwenye album hiyo mastaa kadhaa walikuwepo mfano Frida, Baraka de Prince, One Incridible na wengine.

Album ya mwisho kabla ya Beberu ilikuwa Live at Sauti za busara ambayo ilikuwa na ngoma ambayo ilikuwa na ngoma 14.

Hii ya tatu bado hajaweka wazi itakuwa na ngoma ngapi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii