Urusi inapanua zaidi ushawishi wake barani Afrika. Shirika linalohusika na vituo vya kitamaduni vya Urusi duniani kote limetangaza kusaini makubaliano ya ushirikiano na mashirika ya ndani ambayo tayari yameanzishwa barani humo. Nchi nane za Afrika zinahusika na zitashuhudia kufunguliwa kwa vituo vya kitamaduni vya Urusi.
Vituo vinane vya kitamaduni vya Urusi, vitafunguliwa barani Afrika. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Togo, Mali, Kenya, Madagascar, Sao Tome na PrÃncipe, na Sierra Leone zinatarajiwa kuzindua vituo hivi vipya vya Urusi hivi karibuni, kulingana na miundo iliyopo ya ndani, ambayo itatambuliwa rasmi na kusimamiwa na Moscow.
Mikataba mitano ya ushirikiano ya aina hii tayari ilisainiwa mnamo mwaka 2024. Zaidi ya hayo, kuna matawi tisa ya serikali yanayodaiwa kuwa barani Afrika na Rossotrudnichestvo, shirika la ushawishi la serikali ambalo limekuwa chini ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa miaka minne sasa.
Vituo vya kitamaduni vinavyoshukiwa kuwa vya ujasusi
Lengo kuu la hizi Nyumba za Urusi ni 'kukuza na kuendeleza miradi kuhusu lugha, sayansi, sanaa, na maadili ya Kirusi'." Diplomasia ya kitamaduni, kwa mfano kupitia maonyesho ya filamu, maonyesho ya michezo ya kuigiza (thiyeta), au mafundisho ya lugha. Hata hivyo, taasisi hizi pia zinashukiwa na idara za usalama na ujasusi za Ulaya kufanya shughuli za siri, au hata ujasusi.
Mapema mwezi huu, katika muktadha wa kuongezeka kwa mivutano kati ya Ujerumani na Urusi, tawi la Berlin liamriwa kufungwa. Kremlin ilijibu kwa kuchukua hatua kama hizo dhidi ya taasisi za Ujerumani zilizopo nchini Urusi.