Kamanda mpya ateuliwa kuongoza vita dhidi ya Boko Haram

Nigeria imemteua kamanda mpya kuongoza operesheni za kijeshi dhidi ya wanajihadi wa Boko Haram na Islamic State kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, akichukua nafasi ya mkuu wa operesheni hiyo aliyedumu chini ya miaka miwili baada ya kuteuliwa kwake, msemaji wa jeshi alisema Jumatano.

Uteuzi huo umefanyika wakati nchik hiyo ikijiandaa na uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari mwakani, ambapo suala la ukosefu wa usalama linabaki kuwa moja ya ajenda kubwa ya wagombea baada ya miaka mingi ya vurugu, ujambazi na utekaji nyara katika sehemu mbalimbali za nchi.

Meja Jenerali Ibikunle Ademola Ajose, ambaye hapo awali alihudumu katika Makao Makuu ya Jeshi huko Abuja, anachukua nafasi ya Meja Jenerali Abdulsalam Abubakar, kamanda wa 15 wa Operesheni Hadin Kai, ambaye alichukua wadhifa huo Aprili mwaka 2025.

Uasi wa Boko Haram na makundi wenza yaliyojitenga wameua zaidi ya watu elfu 40 na kuwalazimisha wengine mamilioni kukimbia makazi yao tangu mwaka 2009, hii ni kulingana na takwimu kutoka taasisi ya ACLED.

Utovu wa usalama ulitatiza zoezi la upigaji kura katika sehemu za kaskazini mashariki mwa Nigeria wakati wa uchaguzi uliopita na bado umeendelea kuwa changamoto hata wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwakani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii