Nchini Kenya, maagizo mapya ya serikali yanayolenga kuwafukuza wafanyabiashara wa kigeni wasio na vibali yanaendelea kuzua utata.
Jumanne ya tarehe 8 Septemba ilishuhudia wimbi kubwa la taarifa rasmi na miitikio kutoka kwa ulimwengu wa kisiasa na mashirika ya kiraia. Wote wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya wageni na wanakataa kufuata njia ya Afrika Kusini, ambapo shinikizo kutoka kwa makundi yanayopinga wahamiaji limesababisha kuondoka kwa mamia ya maelfu ya wageni katika miezi ya hivi karibuni. Pia wanahofia madhara hasi kwa nchi hiyo, moja ya wanachama wa EAC, Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wa upinzani wa Kenya, mbinu ya William Ruto iko wazi. Rais anajificha nyuma ya kidole, akijaribu kuwalaumu wageni kwa kushindwa kwa sera yake ya kiuchumi. "Hakuna Mwafrika anayepaswa kuwa mbuzi wa kafara ili kuhalalisha ukosefu wa ajira na mgogoro wa gharama za maisha," anasema Martha Karua wa Chama cha Ukombozi wa Watu. "Sera hii haitegemei sheria yoyote," anaongeza David Maraga, Jaji Mkuu wa zamani wa Mahakama Kuu na mgombea katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2027.
Ahmed Rashi, mgombea katika uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2027 huko Langa'ta, anasema: "Rais Ruto anatumia hoja hii kuchochea utaifa nchini humu, kuwalaumu wageni kwa ukosefu wa ajira kwa maskini. Hajaunda kazi hata moja tangu alipoingia madarakani."
Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) pia inaonyesha wasiwasi wake kuhusu mazingira na namna raia wa kigeni wanavyofukuzwa nchini. Inalaani ukandamizaji wa "jumla", ikisema kwamba hali zinapaswa kutathminiwa kwa msingi wa kesi kwa kesi, na inadai kuwa tayari imepokea malalamiko kutoka kwa wakimbizi.
"Warundi, Waganda, na Watanzania wanachangia zaidi kwa uchumi wa Kenya kulko wananchi wa Kenya"
Kwenye mitandao ya kijamii na runinga za Kenya, hilo ndilo tu lililokuwa likizungumziwa siku ya Jumanne. Odhiambo Ramogi, mkurugenzi wa Elim Capital, kampuni ya uchambuzi wa kiuchumi, anahofia kwa upande wake kuwa hatua hizi zinaweza kudhoofisha nafasi ya Kenya ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambayo pia ni eneo la biashara huru na soko la pamoja. "Rais amekuwa asiyewajibika, mzembe, na mbinafsi. Lazima tuhakikishie EAC ahadi yetu. Warundi, Waganda, na Watanzania wanachangia zaidi Kenya kuliko Wakenya wenyewe. Kwa hiyo tutapoteza mengi tukiendelea kufuata mwelekeo wa chuki dhidi ya wageni tunaolazimishwa na rais." Chama cha Sheria cha Afrika Mashariki pia kinasisitiza wasiwasi wake kuhusu kuheshimiwa kwa mikataba ya kikanda.
Kwa upande wake, serikali ya Kenya inaendelea kushikilia msimamo wake. Esther Muthoni Passaris, mbunge kutoka chama tawala jijini Nairobi, alitangaza siku ya Jumanne, Septemba 8, kwamba ofisi ya rais wa Kenya imetangaza muda wa siku 90 kwa raia wa kigeni wanaofanya biashara nchini humo kuhalalisha nyaraka na vibali vyao vya kisheria.