Ufalme wa Tooro nchini Uganda umemteua mfalme mpya kujaza nafasi hiyo kufuatia kifo cha mtangulizi wake Oyo Nyimba, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 34, moja ya waliokuwa wafalme vijana zaidi duniani.
Katika taarifa kwa vyombo vya Habari, Kamati maalum yenye majukumu ya kuwateuwa wafalme, ilimtangaza mwanaflame Edward Rukidi Kijanangoma kuwa mfalme mpya.
Rukidi ni mhariri na mtangazaji wa telivisheni ya taifa UBC inayomilikiwa na serikali ya Uganda.
Oyo alifariki Agosti 27 akiwa nchini Marekani alipokuwa akipokea matibabu ya saratani ya ubongo.
Oyo Nyimba, balozi wa Umoja wa Mataifa katika vita dhidi ya maambukizo ya Ukimwi, aliteuliwa mfalme mwaka wa 1995 akiwa na umri wa miaka mitatu, akiingia katika vitabu vya kumbukumbu kuwa mfame mdogo zaidi dunaini.
Mwili wa Oyo Nyimba ulirejeshwa nchini Uganda Ijumaa iliopita, na anatarajiwa kuzikiwa Jumamosi ya wiki hii.