Juba yatakiwa kuweka mazingira salama kuelekea uchaguzi mkuu

Watalaam wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wameitaka mamlaka ya Sudan Kusini kuhakikisha inaweka mazingira salama kwa wanasiasa na raia kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba.

Wataalamu hao wameonya kuwa vikwazo vinaweza kuwazuia raia kutoa maoni kwa uhuru pamoja na kuondoa imani yao kwenye mchakato wa uchaguzi.

Katika ujumbe wao, wamewataka viongozi wa Sudan Kusini kuafikiana kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, wakisisitiza kuwa umoja wa wanasiasa unahitajika zaidi ilikuepusha nchi kuingia katika vurugu na kuharibu mchakato wa utekelezwaji wa makubaliano ya amani.

Watalaam hao pia walikutana na mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini Sudan Kusini, mabalozi na wanadiplomasia kutoka katika nchi za Ukanda, mkutano ambao uliangazia mchakato wa amani wa Sudan kusini na maandalizi ya uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake, Umoja wa Afrika umetakiwa kuisiadia Juba kutekeleza makubaliano ya amani kwa ajili ya kuhakikisha uthabiti wa nchi .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii