Kajala Atoa Nukuu Ya Kuwatia Moyo mashabiki Wake

Supastaa wa  Bongo Movies Kajala Masanja  alivuma sana mwaka jana baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Harmonize.

Alizidi kuvuma baada ya wawili hao kuachana, kwani uhusiano wao haukudumu sana.

Kwa muda sasa Kajala amekuwa akitoa nukuu za kuwatia moyo mashabiki wake na hata kuwapa ushauri kwa jambo moja au lingine.

Nukuu mpya kutoka kwa Kajala inawahimiza mashabiki wake wawe makini kutomuumiza mtu yeyote kwani kuna baadhi ya watu ambao hawana watu wa kuwafariji.

“JItahindi usimuumize mtu yeyote, watu wengine hawana watu wa kuwafariji,” anasema Kajala au Mama Pau.

Nukuu nyingine ilizua mjadala kutoka kwa Kajala ni hii; “Unapaswa kuhisi kupendwa bila kuhisi kwamba unaomba kupendwa…

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii