Jaji Chande atoa sababu nne za tume ya Oktoba 29 kuongezwa muda

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio na vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 na baada, Jaji Chande ametoa sababu nne za tume hiyo kuongezewa muda wa siku 21.

Jaji Chande ametoa sababu za kuomba nyongeza hiyo ya muda kuwa ni ukubwa, kina kwa kazi hiyo na ushahidi uliochelewa kuwafikia na ripoti hiyo kutakiwa kuandikwa kwa lugha mbili ya Kiswahili na Kingereza.

" Moja ushahidi mwingi unaendelea kuja, pili ushauri wa kitaalamu ambao tumeuomba wataalamu wa sayansi wanatupa, tatu kuchambua kwa kina, nne kuhakikisha ushahidi huo unakuwa katika lugha mbili za Kiswahili na Kingereza."

Jaji Chande ameyasema hayo leo Aprili 8, 2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini es Salaam.

Aidha, Jaji Chande amesema kuwa awali walipanga kufanya uchunguzi katika mikoa sita lakini wamelazimika kufikia mikoa 12 na kukusanya taarifa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii