Mjumbe mpya wa katibu Mkuu wa UN nchini DRC aanza kazi

Mwanadiplomasia wa Marekani James Swan ameanza kazi rasmi siku ya jumanne kama Mjumbe maalum wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mkuu wa MONUSCO.

Uteuzi wake unakuja huku kukiwa na ukosefu wa usalama unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo, ambapo waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanadhibiti eneo kubwa kwenye majimbo ya Kivu kaskazini na kusini.

Azimio la UN nambari 2808, lililopitishwa Desemba 2025 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeidhinisha mamlaka ya Monusco likifafanua upya vipaumbele vyake kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama huko Ituri, Kivu Kaskazini, na Kivu Kusini, ambapo MONUSCO imepewa jukumu la kufuatilia usitishaji mapigano.

Maandishi hayo pia yanajumuisha mifumo mipya ya kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Amani wa Washington, uliosainiwa Juni 2025 kati ya DRC na Rwanda, na Mkataba wa Amani wa Doha, uliohitimishwa Novemba mwaka huo huo.

Katika muktadha huu, MONUSCO inaombwa kuchukua jukumu kubwa katika kuunga mkono usitishaji mapigano wa kudumu, hasa kupitia utaratibu wa ufuatiliaji na uthibitishaji wa yanayoendelea eneo la mashariki mwa DRC.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii