Iran imesema usalama katika mlango wa Bahari wa Hormuz unaweza kurejea mara moja iwapo Marekani itakubali kutekeleza matakwa yote ya Tehran.
Kauli ya Iran imetolewa na msemaji katika Wizara yake ya mambo ya nje Esmaeil Baghaei, wakati akijibu swali la waandishi wa Habari kuhusu mpango wa siku mbili wa Tehran kuufungua mlango wa Bahari wa Hormuz.
Baghaei amesisitiza kuwa na haki za Iran kuitaka Marekani kuondoa vizuizi kwenye bandari zake, kuondoa vikwazo dhidi yake na kutekeleza makubaliano yalioafikiwa mwezi Juni kwa lengo la kumaliza vita katika pande zote mashariki ya kati.
"Iwapo Marekani itatekeleza yaliokubakuwa, usalama utarejea katika mlango wa Bahari wa Hormuz na ukanda wa mashariki ya kati haraka iwezekanavyo." Amesema Esmaeil Baghaei.
Katika hatua nyengine, Iran imesema haitokubali Marekani kutatiza uchumi wake kwa kuendelea kuweka vizuizi kwenye bandari zake.
Iran vilevile imesema imeweka mipango ya kisiasa, kidiplomasia na kiulinzi kupambana na vikwazo vya Marekani na hatua yake ya kuendeleza kuweka vizuizi kwenye bandari zake.