Wanajeshi wa Libya wauawa katika shambulizi la Ukraine

Maafisa wawili wa jeshi la wanamaji la Libya wamefariki dunia kutokana na majeraha waliyopata katika shambulizi la droni za Ukraine dhidi ya meli ya kivita ya Urusi nchini Libya.

Maafisa hao wawili wamefariki jana Jumanne kutokana na majeraha waliyopata katika shambulizi hilo lililotokea Jumapili dhidi ya meli ya kivita ya Urusi iliyokuwa imetia nanga mashariki mwa Libya, katika kambi ya wanamaji ya Benghazi.

Limesema meli hiyo ilikuwa imetia nanga katika kambi hiyo kwa ajili ya kujaza mafuta na kupokea vifaa vinavyohitajika.

Uongozi wa jeshi hilo umeahidi kulipiza kisasi, ukisema utafanya hivyo kwa wakati na mahali panapofaa, na kwa njia zinazofaa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii