Mzozo wa kisheria kuhusu ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) unaendelea kushika kasi baada ya Morocco kutangaza kuwa itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuirejeshea Senegal ubingwa katika mashindano hayo.
Mzozo wa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) umeingia hatua mpya baada ya Morocco kutangaza rufaa dhidi ya uamuzi wa kuirejesha Senegal kama mabingwa wa mashindano hayo.
Shirikisho la soka la Morocco linadai kuwa kulikuwa na mawasiliano yasiyofaa kati ya mmoja wa waamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) na rais wa shirikisho la soka la Senegal kabla ya hukumu kutolewa, jambo linalozua maswali kuhusu uwazi na uadilifu wa mchakato huo.
Senegal yadai haki imetendeka
Wakati huo huo, Senegal inatupilia mbali madai hayo, huku mvutano ukizidi kuongezeka kufuatia sakata la fainali iliyogubikwa na vurugu na malalamiko ya kiamuzi.
Ama kwa upande mwengine, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limesema linaheshimu uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuhusu sakata la ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), na kusisitiza kuwa litachukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha uamuzi huo unatekelezwa kikamilifu.