UN: KARIBISHA USITISHO WA MAPIGANO KATI YA MAREKANI NA IRAN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amekaribisha tangazo la kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili kati ya Marekani na Iran.

Kupitia msemaji wake, Guterres ametoa wito kwa pande zote kuheshimu masharti ya makubaliano hayo na sheria za kimataifa, akisisitiza kuwa sitisho hilo ni la muhimu kulinda maisha ya raia na kupunguza mateso ya kibinadamu yanayosababishwa na vita.

Aidha, Katibu Mkuu amethamini juhudi za upatanishi zilizofanywa na nchi mbalimbali, ikiwemo Pakistan, katika kufanikisha makubaliano hayo, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kufanikisha amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii