Tangazo la kusitisha mapigano kwa wiki mbili lililotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, linaitaka Iran kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.
Hata hivyo, mchambuzi wa usafirishaji wa meli, Lars Jensen, amesema bado hakuna mabadiliko makubwa yaliyojitokeza katika eneo hilo, akibainisha kuwa itachukua muda kurejesha uaminifu miongoni mwa wadau wa usafirishaji.
Akizungumza na vyombo vya habari nchini humo ambapo amesema kuwa anatarajia kuona meli zikianza kutoka katika Ghuba katika siku chache zijazo, lakini kwa tahadhari kubwa.
Hata hivyo ameongeza kuwa hali hiyo itakuwa ni “mtiririko wa tahadhari” (trickle flow), kwani wamiliki wa meli wana hofu ya meli zao kukwama endapo makubaliano ya kusitisha mapigano yatavunjika, hali inayodhihirisha kuwa bado kuna sintofahamu kuhusu usalama wa eneo hilo muhimu la biashara ya kimataifa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime