Museveni ,Kikwete wazungumza amani Sudan Kusini

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu, Jakaya Mrisho Kikwete, katika Ikulu ndogo ya Nakasero jijini Kampala.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili hali ya kisiasa na kiusalama nchini Sudan Kusini, wakisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya amani na maridhiano ili kurejesha utulivu wa kudumu.

Yoweri Kaguta Museveni alieleza kuwa Uganda itaendelea kuunga mkono juhudi zote za kuleta amani nchini humo, akibainisha kuwa utulivu wa maeneo kama Equatoria, yenye idadi kubwa ya raia wa Uganda, ni muhimu kwa usalama wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi.


Kwa upande wake, Jakaya Mrisho Kikwete, aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika, ameendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kikanda na juhudi za upatanishi katika kutatua migogoro, akitumia uzoefu wake mkubwa wa kidiplomasia barani Afrika.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii