Zaidi ya watu 70 wameuawa kwenye shambulio kwenye timbo Sudan Kusini

Watu  zaidi ya 70 wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya  dhahabu Khor Kaltan, nchini Sudan Kusini.

Shambulizi hili lilitekelezwa na watu wenye silaha ambao hawajafahamika.

Makamu wa rais James Wani Igga shambulio hilo limetokea kilomita 70 kusini magharibi mwa mji mkuu Juba, na kusababisha vifo vya watu 73 na kuwajeruhi wengine 25;

Wakati huu uchunguzi ukiendelea kubaini waliohusika, vikosi vinavyohusiana na  aliyekuwa Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar vinatuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Hata hivyo, wandani wa Machar ambaye kwa mwaka mmoja amezuiwa nyumbani huku akikabiliwa na kesi ya uhaini, wanakanusha madai hayo na badala yake kuwashtumu wanajeshi wa serikali chini ya rais Salva Kiir kwa kuhusika.

Tangu kupata uhuru wake mwaka 2011, Sudan Kusini imekabiliwa na misururu ya ghasia za mara kwa mara, mara nyingi zikichochewa na uhasama wa kisiasa. 

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii