Bei ya mafuta yapanda hadi Dola 115 kutokana na vita ya Iran

Bei ya mafuta duniani imeendelea kupanda na kufikia zaidi ya dola 115 kwa pipa katika masoko ya Asia, kufuatia kuongezeka kwa mvutano wa vita kati ya Marekani, Israel na Iran, ambayo sasa imeingia zaidi ya mwezi mmoja.


Aidha ripoti zinaonyesha kuwa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya mafuta na usafirishaji, ikiwemo hatari katika njia muhimu kama Ghuba ya Hormuz, yameathiri upatikanaji wa nishati na kusukuma bei kupanda .

Hata hivyo hali hii inaendelea kuongeza presha kwenye uchumi wa dunia huku hofu ya mfumuko wa bei ikiongezeka.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii