Iran imeingia siku ya 32 tangu kukatika kwa mtandao, huku watumiaji wengi wakikosa mawasiliano nje ya mtandao kwa zaidi ya saa 744, kwa mujibu wa taasisi ya ufuatiliaji wa mtandao, NetBlocks.
Inaelezwa kuwa kiwango cha mawasiliano ya intaneti na mataifa ya nje kimesalia kwenye asilimia 1 tu ya hali ya kawaida.
Aidha baadhi ya maafisa wa serikali, watumiaji wanaoiunga mkono serikali pamoja na baadhi ya waandishi wa habari bado wana uwezo wa kutumia mtandao bila vikwazo, wakati wengine wakilazimika kulipa fedha nyingi ili kuweza kupata huduma hiyo.
Watu wachache wamefanikiwa kuunganisha mtandao kwa kutumia huduma za intaneti ya satelaiti kama Starlink na njia nyingine, lakini gharama zake ni kubwa.
Hata hivyo nchini Iran, kutumia au kumiliki huduma ya Starlink kunaweza kusababisha kifungo cha hadi miaka miwili gerezani, huku mamlaka zikiongeza juhudi za kukabiliana na matumizi yake.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime