Bunge Laahirishwa Dakika 15 ili kupisha mazishi ya Lukuvi

Kikao cha kwanza cha Mkutano wa Tatu wa Bunge la 13 la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoanza leo Machi 31, 2026 jijini Dodoma kimeahirishwa baada ya kudumu kwa dakika 15 pekee hadi kesho Aprili 1, 2026 saa 3:00 asubuhi.


Aidha kuahirishwa huko kumetokana na kutokuwepo kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba aliyekuwa anatarajiwa kuwasilisha bajeti, ambapo yupo kwenye shughuli za mazishi ya aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Isimani, William Vangimembe Lukuvi.

Hata hivyo bunge hilo linatarajiwa kujadili na kupitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii