Wafungwa 11 wamepoteza maisha na wengine wameambukizwa kipindupindu baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa huo katika gereza la Mbanza-Ngungu katika mkoa wa Kongo Central nchini DRC.
Wizara inayoshughulikia masuala ya Haki, imethibitisha kupoteza maisha kwa wafungwa hao, baada ya kubainika kuwa wafungwa hao wamekuwa wakilala kwenye sakafu na hawakuwa na maji safi ya kunywa.
Mlipuko katika gereza hilo lililojengwa na Wakoloni kutoka Ubelgiji, ulithibitishwa Machi tarehe 27 kwa mujibu wa Waziri wa masuala ya Haki Guillaume Ngefa ambaye ameongeza kuwa wengine 74 wameambukizwa.
Gereza hilo lililo umbali wa Kilomita 150 kutoka jijini kuu Kinshasa, ni miongoni mwa magereza ambayo yana mrundikano mkubwa wa wafungwa ambapo kwa sasa ina wafungwa 800 hali ambayo inaendelea kuhatarisha maisha yao.
Serikali inasema imewatuma maafisa wa afya kwenye gereza hilo, huku hatua zikichukuliwa kuhakikisha kuwa wafungwa wanapata maji safi ya kunywa na kuzuia ongezeko la wafungwa katika gereza hilo.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime