Mataifa Yaongeza Onyo la Safari Kufuatia Mvutano wa Marekani na Iran

Nchi kadhaa, ikiwemo Marekani, zimeongeza tahadhari za usafiri na kuanza kuwaondoa wafanyakazi wasio wa lazima kutoka balozi zao Mashariki ya Kati, kufuatia kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na Iran.

Australia, India, Sweden, Singapore na Cyprus zimewaonya raia wao kuepuka safari za Iran na baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati, huku waliopo wakishauriwa kuwa tayari kuondoka endapo hali itazidi kuwa tete.

Marekani pia imewaondoa wafanyakazi na familia zao kutoka baadhi ya balozi zake, ikisisitiza hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa raia wake.

Mvutano huo umechochewa na msimamo mkali wa Washington kuishinikiza Tehran kusitisha programu zake za nyuklia na silaha, huku Iran ikionya kuwa itajibu vikali endapo itashambuliwa.

Hata hivyo hali hiyo imeibua hofu ya kuongezeka kwa vurugu au mashambulizi ya kijeshi ikiwa juhudi za kidiplomasia hazitazaa matunda.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii