Wakazi wa Mkoa wa Simiyu wameiomba Serikali kupitia Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupozea umeme ili kupata huduma ya uhakika na kuepuka changamoto za mara kwa mara za kukatika kwa umeme.
Ambao wakazi hao wamesema tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa likizuia shughuli zao za kiuchumi na kuathiri mapato yao.
Aidha wameeleza matumaini kuwa kukamilika kwa kituo hicho kutaondoa changamoto mbalimbali na kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu ya umeme wa uhakika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha, amesema wawekezaji, hususan wa viwanda, wanahitaji umeme wa uhakika ili uwekezaji wao upate tija, jambo litakalosaidia kuongeza pato la taifa kupitia uzalishaji wa viwanda.
Hata hivyo ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni florenciaPeter tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime