Wizara ya Afya Yatoa Tahadhari Kuhusu Mafua, UVIKO-19 na Dengue

Wizara ya Afya imewataka wananchi kuchukua tahadhari kufuatia ongezeko la wagonjwa wa mafua makali ya Influenza na UVIKO-19, huku ikisisitiza kuchukua hatua za kinga ili kudhibiti maambukizi.

Tahadhari hiyo imekuwa muhimu hasa wakati huu wa mabadiliko ya msimu, ambapo kuna ongezeko la magonjwa yanayohusiana na njia ya hewa kama homa, kukohoa na baridi.

Aidha, serikali imeonya kuhusu hatari ya Homa ya Dengue kutokana na mvua za masika zinazochochea uzalishaji wa mbu aina ya Aedes.

Pia, Wizara imetaja kuwa nchi ipo katika mlipuko wa Kipindupindu, ambao umeathiri mikoa yote isipokuwa Kilimanjaro na Njombe, ambapo visa vimekuwa vikiongezeka kwa takriban mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo taarifa hiyo imetolewa leo Februari 25, 2026, na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Grace Magembe, akiweka mkazo kwa wananchi kuchukua tahadhari na hatua za kinga.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii