Serikali Yaimarisha Mfumo wa Stakabadhi, Choroko Yapaa Bei

Serikali imewataka wakulima na wafanyabiashara kuendelea kuunga mkono Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ili kuongeza tija na uhakika wa masoko huku ikiahidi kuboresha upatikanaji wa pembejeo, mbegu bora, teknolojia za kisasa na masoko ya mazao.

Ambapo waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ameyasema hayo leo Februari 25, 2026 baada ya kushuhudia mnada wa choroko katika Ghala Teule la Ndilima, Hungumalwa mkoani Mwanza.

Aidha ameeleza kuwa amefurahishwa na kupanda kwa bei ya zao hilo kutoka Sh1,200 kwa kilo mwaka jana hadi Sh1,600 msimu wa 2025/26, hatua inayodhihirisha mafanikio ya mfumo huo.

Kwa upande wao, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) na COPRA zimetakiwa kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wakulima kuanzia uzalishaji hadi uuzaji.

Hata hivyo viongozi wa Wilaya ya Kwimba na wabunge wa eneo hilo wamesema mfumo huo umeleta uwazi wa bei na soko la uhakika, huku wakisisitiza kupunguzwa kwa tozo ili kuongeza faida kwa wakulima wa choroko.

Sasa ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Evance Mlyakado tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. 

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii