Tanzania Yasajili Dawa ya Lenacapavir Kudhibiti VVU

Serikali ya Tanzania imesajili rasmi dawa ya Lenacapavir kwa ajili ya kudhibiti na kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), hatua inayotarajiwa kuboresha tiba na kinga dhidi ya maambukizi hayo nchini.

Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi, amesema dawa hiyo tayari imetambuliwa na kusajiliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), huku mchakato wa kuiingiza rasmi kwenye matumizi ya kitaifa ukiendelea kupitia mapitio ya miongozo ya matibabu.

Lenacapavir ni dawa ya sindano inayozuia maambukizi ya VVU, yenye uwezo wa kutumika kama mbadala wa ARV’s kwa wenye maambukizi.

Katika jaribio la utafiti lililofanywa Uganda mwaka 2025, dawa hiyo ilionyesha ufanisi wa asilimia 100. Mchakato wa kuipatia mwongozo wa kitaifa umekamilika tayari, na dawa itaanza kutumika kama sehemu ya mpango wa kudhibiti VVU nchini.

Hata hivyo ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni florenciaPeter tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. 

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii